Katika taarifa yake ya Alhamisi jioni, Al-Azhar iliashiria kuuawa Shahidi Mashahidi waliotolewa mhanga kupitia jinai za watenda jinai mazayuni na kubainisha kuwa: Utawala wa Israel ulileta uharibifu na ufisadi mkubwa katika ardhi yetu ya Kiarabu, na umefanya mauaji, uharibifu, na kukalia kwa mabavu ardhi za zetu, utekaji nyara na kufanya uharibifu a kila aina mbele ya macho na masikio ya nchi zisizo na utashi na na uwezo, na zisiokuwa na mawazo (fikra), na mbele ya macho ya Jumuiya ya Kimataifa ambayo imezama katika ukimya kama ukimya wa wafu kaburini. Thamani ya Sheria ya Kimataifa haifikii wala kulingana sawa na bei ya ule wino ulioandika sheria hiyo.
Al-Azhar amesisitiza kuwa: Mashahidi wa Muqawama wa Palestina walikuwa wapiganaji halisi wa Muqawama (Upinzani) na waliweka hofu na woga katika nyoyo za adui.
Al-Azhar akaendelea kusema: “Mashahidi wa Upinzani (Muqawamah) wa Palestina, walisapoti (walihami), walipigana jihadi, walishikilia ardhi ya nchi yao hadi Mwenyezi Mungu alipowakadiria kuuliwa Kishahidi katika kuzima njama na uchokozi wa adui na kuilinda ardhi yao tukufu na suala lao na letu (la Palestina), ambalo ni suala la Waarabu na Waislamu wote katika Mashariki na Magharibi ya Dunia.
Katika muendelezo wa kauli hiyo: Al-Azhar sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa kuuliwa kwa “Mashahidi wa Muqawama wa Palestina” inasisitiza umuhimu wa kufichua uwongo na ulaghai wa chombo cha habari cha Kizayuni na juhudi zake za kupotosha nembo za Muqawamah wa Palestina katika akili za vijana wetu na watoto wetu na katika kujumuisha Mashahidi hao kama Magaidi.
Al-Azhar alisisitiza: "Upinzani, ulinzi wa nchi, ardhi na suala la kufa (kishahidi) kwa ajili ya hilo, ni suala la heshima ambapo ni kama vile hakuna kitu kingine chochote kile (ispokuwa kuipata heshima hiyo)."
Israel ilitangaza Alhamisi kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sin’war wakati wa mapigano katika Mji wa Rafah, ikidai kuwa operesheni hiyo haikumlenga yeye, lakini vikosi vyake vilimgundua "Kwa ghafla na kubahatisha".